NAMBA YA SIMU YA IGGY AZALEA YAWEKWA WAZI SABABU YA PIZZA

NAMBA YA SIMU YA IGGY AZALEA YAWEKWA WAZI SABABU YA PIZZA

Like
483
0
Monday, 09 February 2015
Entertanment

Rapa kutoka nchini marekani Iggy Azalea huenda ataifungulia mashtaka kampuni Papa John maarufu nchini humo kwa uuzaji wa pizza

Hatua hiyo inakuja mara baada ya mmoja wa madereva wa kampuni hiyo aliyepewa kazi yakumpelekea pizza rapa huyo kugawa namba hiyo kwa mdogo wake mmoja ambapo baadae mdogo wa dereva huyo alimtumia ujumbe mfupi Iggy na kumfahamisha kuwa namba hiyo alipewa na kaka yake na kuongeza kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa rapa huyo

Iggy Azalea alichukua hatua ya kuwasiliana na bosi wa kampuni ya Papa John kwa kumuomba picha za madereva waliokuwa zamu siku hiyo hata hivyo hakupata ushirikiano wowote ndipo alipochukua hatua ya kushare taarifa hiyo kwenye akaunti yake ya twitter kwa kuelezea kusikitishwa kwake na kampuni hiyo

iggy

Comments are closed.