NANYUMBU WALALAMIKA KUNYANYASWA HOSPITALI MASASI

NANYUMBU WALALAMIKA KUNYANYASWA HOSPITALI MASASI

Like
431
0
Thursday, 27 November 2014
Local News

WANANCHI wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wamemlalamikia Katibu Mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA kuwa wagonjwa wanaotoka wilani humo kwenda Hospital ya Wilaya ya Masasi wananyanyaswa.

Wananchi hao wameiomba Serikali kutoa kibali cha kupandisha hadhi hospital ya Wilaya ya Nanyumbu ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kibali kwa muda mrefu lakini hadi sasa imeshindwa kutoa na matokeo yake hospital ya Wilaya ya Nanyumbu imebaki kuwa Kituo cha Afya.

Wananchi hao wamemwambia Ndugu KINANA kuwa ni vema akawasaidia kuiambia serikali kuharakisha utoaji wa kibali cha kupandisha hadhi kituo cha Afya cha Mangaka kuwa hospital ya Wilaya kwani ina vigezo vya kutosha.

Comments are closed.