NASA: TOKYO NA SINGAPORE MIONGONI MWA MAENEO YANAYOHOFIWA KUZAMA BAHARINI

NASA: TOKYO NA SINGAPORE MIONGONI MWA MAENEO YANAYOHOFIWA KUZAMA BAHARINI

Like
215
0
Friday, 28 August 2015
Global News

UTAFITI mpya uliyofanywa na shirika la utafiti wa safari za anga la Marekani NASA, unaonyesha kuwa kuongezeka kwa kina cha maji baharini kwa zaidi ya mita moja katika kipindi cha miaka 100 hadi 200 ijayo hakuzuwiliki.

Kuongezeka huko kunatishia kuyazamisha maeneo na miji mikubwa duniani iliyoko chini ya usawa wa kina cha bahari kama Tokyo na Singapore.

Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha utafiti cha NASA Michael Freilich, zaidi ya watu milioni 150, wengi wao kutoka bara la Asia, wanaishi ndani ya mita moja tu juu ya usawa wa sasa wa bahari.

Comments are closed.