NDEGE ILIYOANGUKA MISRI ILILIPULIWA

NDEGE ILIYOANGUKA MISRI ILILIPULIWA

Like
208
0
Tuesday, 17 November 2015
Global News

NCHI ya Urusi imethibitisha kuwa ajali ya ndege ya Metrojet iliyoanguka na kuua watu zaidi ya 200 katika rasi ya Sinai nchini Misri mwezi uliopita iliangushwa na shambulio la kigaidi.

Mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Alexander Bortnikov amemueleza rais wa nchi hiyo Vladimir Putin kuwa ndege hiyo iliangushwa na bomu lenye uzani wa kilo moja.

Bortnikov alipokamilisha maelezo yake kwa rais Putin, rais huyo pamoja na mawaziri wengine wakuu wamesimama na kunyamaza kimya kwa muda kabla ya rais Putin kuapa kulipiza kisasi na mashambulizi zaidi nchini Syria.

Comments are closed.