NDEGE YA KWANZA ISIYO NA RUBANI YA PAKISTAN YAFANYA SHAMBULIO

NDEGE YA KWANZA ISIYO NA RUBANI YA PAKISTAN YAFANYA SHAMBULIO

Like
253
0
Monday, 07 September 2015
Global News

NDEGE ya kwanza isiyo na rubani iliyotengenezwa nchini Pakistan imewashambulia na kuwauwa watu watatu wanaoshukiwa kuwa waasi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo hii leo.

Kawaida, ndege za aina hiyo za Kimarekani ndizo hufanya mashambulizi kwenye mkoa wa Waziristan karibu na mpaka wa Afghanistan, lakini sasa jeshi la Pakistan limeanza kutumia ndege zake kwenye eneo la Bonde la Shawal.

Ndege hiyo ilijaribiwa mara ya kwanza mapema mwaka huu, lakini operesheni zake zikasitishwa baada ya wasiwasi kuzuka juu ya uhakika wake.

Comments are closed.