NDEGE YA TAIWAN YAANGUKIA MTONI

NDEGE YA TAIWAN YAANGUKIA MTONI

Like
193
0
Wednesday, 04 February 2015
Global News

NDEGE inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei.

Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa.

Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung. Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo.

Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.

 

Comments are closed.