NDESAMBURO ATARAJIWA KUPELEKA HOJA BINAFSI BUNGENI KUHUSU MAUAJI YA JAMES JOHN

NDESAMBURO ATARAJIWA KUPELEKA HOJA BINAFSI BUNGENI KUHUSU MAUAJI YA JAMES JOHN

Like
323
0
Wednesday, 08 April 2015
Local News

MBUNGE wa Moshi Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, PHILEMON NDESAMBURO, anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuhusu mauaji ya JAMES  JOHN.

Katika hoja hiyo,NDESAMBURO anatarajia kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuliambia Bunge sababu zinazolifanya Jeshi la Polisi kushikwa na kigugumizi kuwakamata watuhumiwa waliohusika katika mauaji hayo.

JOHN, ambaye alikuwa meneja wa Baa na Car wash ya Mo-Town iliyopo Mjini Moshi Mjini,anadaiwa kutekwa June 09 mwaka 2009 na Ndugu Wanne wakiongozwa na kaka yao aitwaye JOHN KISOKA maarufu kwa jina la Magazeti,mfanyabiashara wa jijini Mwanza na kwenda kumtesa kwa kiwango cha juu hadi kufariki dunia.

 

Comments are closed.