Ndoa ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ Hatari

Ndoa ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ Hatari

Like
2226
0
Saturday, 19 May 2018
Entertanment

Prince Harry na mchumba wake Meghan Markle.

MAMILIONI ya watu duniani leo wanatarajiwa kushuhudia ndoa ya kifahari ya mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ na mwigizaji maarufu wa Marekani, Meghan Markle.

Harry akiwasalimia mamia ya watu waliofika kushuhudia ndoa yake.

 

Harry ni mtoto wa Prince Charles wa Uingereza ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili. Prince Charles ambaye ndiye mfalme-mtarajiwa, anajulikana pia kama Prince of Wales.

Ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa katika Kasri la St George, eeo la Windsor, jijini London ambapo inakadiriwa tukio la kufunga ndoa kanisani litahudhuria na watu 1,200 ambao ni jozi 600 za waume na wake zao watakaoshuhudia hafla hiyo viunga vya kasri hilo.

Harry akiingia na kaka yake, Prince William.

 

Vilevile watu zaidi ya 100,000 watajipanga kwenye barabara za eneo hilo wakiwa na bendera za nchi hiyo kuwatakia pongezi wanandoa hao baada ya kutoka kanisani. Prince Charles atamsindikiza Prince Harry katika ndoa yake na Markle kwenye madhabahu ya Kasri hilo wakati baba wa Markle, Thomas, hatohudhuria harusi hiyo kutokana na kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Meghan na mama yake.

 

Meghan na Prince Harry jana walitumia muda wao kukaa na familia zao katika maandalizi ya mwisho. Harry alitumia muda mwingi wa jioni kukaa na kubadilishana mawazo na msimamizi wake (mpambe) ambaye ni Prince William.

Kwa upande wa Markle,mwenye umri wa miaka 36, atasindikizwa kwenda kanisani na Ragland. Pia atakutana na wapambe wengine wa harusi wa kike na kiume ambao ni pamoja na mpwa wa Harry mwenye umri wa miaka minne aitwaye Prince Charlotte, pamoja na watoto wasimamizi wa kidini wa Markle.

Kwa upande wa pete ya harusi hiyo itatokana na pete ya ndoa ya mwaka 1923 ya mama wa Malkia Elizabeth wa Pili iliyotokana na dhahabu ya Ki-Welsh ambapo sehemu yake imekuwa ikituika katika kila pete ya ndoa za jamii ya kifalme.

Kuna tetesi kwamba pete ya Markle huenda ikawa ndiyo ya mwisho kutokana na pete hiyo ya kihistoria. Vilevile, kutokana na fahari ya kijeshi aliyo nayo Prince Harry ni dhahiri atavaa sare zake za kijeshi.

Kutokana na utaratibu wake wa kuwashirikisha wanajeshi katika hafla mbalimbali, panategemewa kuwepo zaidi ya askari 250 kutoka vikosi mbalimbali vilivyo na uhusiano na Prince huyo.

Katika harusi zote za kifalme tangu enzi za Malkia Victoria mwaka 1840, biharusi wote wamekuwa wakivaa nguo za rangi nyeupe, na pamoja na kwamba gauni la Markle bado linafanywa kuwa siri kubwa, bado panategemewa kwamba litakuwa na rangi ileile.

Makao ya Kensington yamethibitisha pia kwamba Prince Harry na Markle watafuata utaratibu wa siku nyingi ulioanza kutumika tangu enzi za Malkia Victoria, yaani kutumia farasi wa rangi ya kijivu wa Windsor kwa kuvuta gari la harusi.

Na iwapo hali ya hewa itakuwa nzuri, inasemekana wanandoa hao watapita katika eneo la Mji la Windsor katika moja ya magari maalum ya kifalme yanayojulikana kama Ascot Landau.

Hata hivyo, kuna baadhi ya wanasiasa mashuhuri ambao hawamo miongoni mwa washiriki wa harusi hiyo.

Nao ni pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Teresa May, na marafiki za Prince Harry ambao ni rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle.

Harusi itaongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby katika kanisa la Mt. George na shughuli yote hiyo itatangazwa kwa mamilioni ya watu duniani kote.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *