NDUGAI: DENI LA MSD LIPO KATIKA UTEKELEZAJI

NDUGAI: DENI LA MSD LIPO KATIKA UTEKELEZAJI

Like
271
0
Monday, 10 November 2014
Local News

NAIBU SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  JOB NDUGAI, amewataka wabunge kuliacha suala la deni la Serikali inalodaiwa na Bohari ya Dawa nchini-MSD, kwakuwa lipo katika hatua za utekelezaji utakaoenda sanjari na utoaji wa ripoti juu ya suala hilo.

 

NDUGAI amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya hoja iliyoibuliwa na mbunge wa Nkasi mashariki mheshimiwa ALLY MOHAMED KESSY alipohitaji kujua nini utekelezaji na mikakati ya serikali katika suala hilo sanjari na suala la Rais kutibiwa nje ya nchi.

 

Kuhusu suala la Raisi kutibiwa nje ya nchi Mheshimiwa KESI amesema kuwa hii inatokana na serikali kutokuwa makini katika kushughulikia mambo muhimu ikiwemo upatikanaji wa dawa za kutosha katika hospitali zilizopo nchini hali inayosababisha huduma kutokidhi viwango vinavyotakiwa.

 

 

 

 

Comments are closed.