KUFUATIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi -NEC-kutangaza kuanza kwa Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa Kutumia Tekinolojia mpya, Mbunge wa Mchinga kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi -CCM SAID MTANDA amesisitizia Tume kuzingatia vigezo sahihi katika maboresho ya daftari hilo.
Akizungumza na EFM kwa njia ya simu amesema umuhimu wa kuboresha Daftari hilo haupo tu katika kuongeza idadi ya wapiga kura bali pia kuondoa watu ambao wamepoteza sifa za kupiga kura kama waliofariki na watu ambao wanatumikia vifungo kwa makosa mbalimbali.