NEC KUWEKA WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA UNGUJA NA PEEMBA

NEC KUWEKA WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA UNGUJA NA PEEMBA

Like
226
0
Monday, 31 August 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kuanzia Septemba 3 hadi hadi 7 mwaka huu ili Umma uweze kupata nafasi ya kulikagua Daftari hilo na kutoa taarifa za kufanyiwa marekebisho pale inapostahili.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume hiyo nchini imesema kuwa Daftari hilo litawekwa wazi katika Ofisi za Shehia zilizopo Unguja na Pemba kisiwani Zanzibar.

 

Wakati wa uhakiki Mpiga kura anaweza kuhakiki taarifa zake kutumia simu ya mkononi kupitia namba husika au tovuti ya Tume  ili kama kuna mapungufu yaweze kufanyiwa kazi kabla ya kuchapisha Daftari la mwisho litakalotumika siku ya Uchaguzi.

 

 

Comments are closed.