NEC YAANZA KUPOKEA FOMU ZA UTEUZI ZA VYAMA 13 LEO

NEC YAANZA KUPOKEA FOMU ZA UTEUZI ZA VYAMA 13 LEO

Like
207
0
Friday, 21 August 2015
Local News

TUME ya Taifa ya uchaguzi Makao makuu, leo imeanza kupokea fomu za uteuzi za vyama 13 kwa ajili ya uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa nchini mwezi oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, Zoezi hilo limeanza leo saa tatu asubuhi na chama cha UPDP na saa tano hiii ni zamu ya Mgombea wa Chama cha Mapinduzi –ccm baada ya mgombea wa Chadema kufanya hivyo saa nne asubuhi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani amesema uchaguzi mkuu wa Mwaka huu utahusisha majimbo mapya 25 na kata 620 ambazo zimeongezeka kutokana na sababu za kiutawala na kuongezeka kwa Idadi ya watu.

Comments are closed.