NEC YABAINI ZAIDI YA WATU ELFU HAMSINI NA MBILI WALIJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA

NEC YABAINI ZAIDI YA WATU ELFU HAMSINI NA MBILI WALIJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA

Like
239
0
Monday, 24 August 2015
Slider

WAKATI Zoezi la kuhakiki taarifa kwa waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura likitarajiwa kukamilika leo Tume ya Taifa ya uchaguzi –NEC- imesema kuwa imebaini zaidi ya watu Elfu 52 waliojiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari hilo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani amesema kuwa ingawa Zoezi hilo limepitia changamoto nyingi lakini limefanikisha lengo lililowekwa kwa kiasi kikubwa.

Aidha amewataka watanzania kutoyumbishwa na maneno yanayotolewa na baadhi ya watu na yasiyo na ukweli wowote juu ya mfumo wa BVR kwani mfumo huo umetumika kwa kuandikisha tu na sio kupigia kura.

Comments are closed.