NEC YAKABIDHI CHETI CHA USHINDI KWA MAGUFULI

NEC YAKABIDHI CHETI CHA USHINDI KWA MAGUFULI

Like
185
0
Friday, 30 October 2015
Local News

KUFUATIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-kumtangaza mgombea wa chama cha mapinduzi-CCM-dokta John Pombe Magufuli kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga wamempongeza kwa kupata ushindi huo.

Dokta Magufuli amekabidhiwa cheti cha ushindi leo Jijini Dar es salaam kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC.

Hafla ya kukabidhiwa cheti imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete.

Comments are closed.