NEC YAKABIDHI RASMI CHETI CHA USHINDI KWA MAGUFULI

NEC YAKABIDHI RASMI CHETI CHA USHINDI KWA MAGUFULI

Like
196
0
Friday, 30 October 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania-NEC-leo imekabidhi rasmi cheti kwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi-CCM-Dokta John Pombe Magufuli sanjari na makamu wa Rais Mteule Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva amesema kuwa wameridhishwa na mchakato mzima wa kutangaza matokeo hali iliyosababisha kumpata mshindi kwa haki.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliohudhuria Hafla ya kukabidhi vyeti hivyo, Mgombea Urais wa ACT Wazalendo Anna Mghwira amesema kuwa atahakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha kwa manufaa ya Taifa.

Comments are closed.