NEC YAONGEZA SIKU 4 ZA KUJIANDIKISHA NA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA

NEC YAONGEZA SIKU 4 ZA KUJIANDIKISHA NA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA

Like
302
0
Thursday, 30 July 2015
Local News

TUME ya taifa ya uchaguzi –NEC– imeongeza siku nne za kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura kwa wakazi wa Dar es salaam kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi  ulioonekana katika vituo mbalimbali vya uandikishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu DAMIAN LUBUVA amesema kuwa hali hiyo imetokana na uwepo wa Idadi kubwa ya watu ambao bado hawajaandikishwa na wanahitaji kuandikishwa.

Jaji Mstaafu LUBUVA amebainisha kuwa takwimu zinaonesha hadi kufikia jana jumla ya wananchi milioni 18, laki nane na ishirini na sita mia saba kumi na nane wameshaandikishwa katika Daftari hilo.

Comments are closed.