MTANDAO wa Asasi za Kiraia wa Kuangalia Chaguzi Tanzania-TACCEO unaoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu umeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye mikoa mingine wakati wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepuka kufanya makosa hayo katika mkoa wa Dar es Salaam hapo kesho.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa mtandao huo MARTINA KABISANA amesema kuwa ni vyema NEC ikahakikisha inatatua mapema changamoto ya kuharibika kwa mashine za BVR kwa mkoa wa Dar es Salaam kama ilivyotokea katika mikoa mingine.
Amebainisha kuwa NEC inatakiwa kuepuka kubadilisha ratiba ya uandikishaji mara kwa mara katika mkoa huo ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu kwenye zoezi zima la uandikishaji.