NEC YAWATAKA WANANCHI KUHAKIKI TAARIFA SIKU 8 KABLA YA UCHAGUZI

NEC YAWATAKA WANANCHI KUHAKIKI TAARIFA SIKU 8 KABLA YA UCHAGUZI

Like
244
0
Tuesday, 13 October 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC– imewaasa  wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya kupigia kura siku nane kabla ya uchaguzi.

 

Hayo yamesema jana  na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa jijini Dar es Salaam.

 

Katika mkutano huo Jaji Mstaafu Lubuva amewasihi viongozi hao kunadi sera zao majukwaani na sio kuilalamikia Tume katika majukwaa  wakati wa kampeni  pia amewataka wanasiasa hao  kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia kutoa taarifa zisizo za kweli kwa waandishi wa habari.

Comments are closed.