NEC YAWATAKA WANANCHI KUTOPOTOSHWA NA MANENO YA WANASIASA

NEC YAWATAKA WANANCHI KUTOPOTOSHWA NA MANENO YA WANASIASA

Like
180
0
Wednesday, 28 October 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imewataka wananchi kutopotoshwa na maneno ya wanasiasa juu ya matokeo ya nafasi ya Urais yanayotolewa na Tume hiyo kuwa yana upendeleo suala ambalo halina ukweli wowote.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo kabla ya kuanza kutangaza matokeo, mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume inatangaza matokeo kwa mujibu wa taratibu na namna yanavyoifikia.

Mbali na hayo Jaji Mstaafu Lubuva ameviasa vyama vya siasa kutoendelea kuwapotosha watanzania kwani matokeo yote ni halali na hakuna upendeleo kwa chama chochote.

Comments are closed.