NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Like
513
0
Thursday, 18 February 2016
Local News

BARAZA la mitiani Tanzania NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 , ambapo  ufaulu  unaelezwa kushuka  kwa asilimia 1.85  kutoka  asilimia 69.75  mwaka 2014  hadi asilimia 67.91 kwa  mwaka  2015.

 

Katibu Mtendaji wa NECTA Dokta Charles Msonde ameeleza kuwa  takwimu za matokeo zinaonesha kuwa bado ufaulu wa masomo yaliyomengi upo chini ya asilimia hamsini na idadi ya watahiniwa waliopata daraja la kwanza, daraja la pili na daraja la tatu ni takribani robo ya watahiniwa waliofanya mtihani.

Aidha, Dokta Msonde amefafanua kuwa baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 87 waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mtihani lakini pia limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 23 ambao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo ya kiafya.

Comments are closed.