NEMA FOUNDATION YATOA MSAADA WA MASHUKA KATIKA BAADHI YA HOSPITALI DAR

NEMA FOUNDATION YATOA MSAADA WA MASHUKA KATIKA BAADHI YA HOSPITALI DAR

Like
279
0
Tuesday, 08 December 2015
Local News

TAASISI isiyo ya kiserikali ya- NEMA FOUNDATION imetoa msaada wa mashuka miamoja katika  baadhi ya hospitali  za Jijini Dar es salaam ikiwemo hospitali ya Mwananyamara ikiwa  ni sehemu  ya utaratibu wao ambao wanaufanya kila mwaka.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo  Bi Mariam  Dedes amesema kuwa wameguswa kutoa misaada hiyo kwa kutambua changamoto mabalimbali zinazo ikabili sekta ya Afya.

Kwa upande wake Mbunge wa kinondoni Muheshimiwa  Mahulid  Mtulya ameishukuru taasisi hiyo na kuziomba taasisi nyingine kujitokeza kutoa misaada kwenye  hospitali hiyo kwani bado  inakabiliwa na changamoto nyingi.

Comments are closed.