NETANYAHU AMTUHUMU BAN KI-MOON KUUNGA MKONO UGAIDI

NETANYAHU AMTUHUMU BAN KI-MOON KUUNGA MKONO UGAIDI

Like
228
0
Wednesday, 27 January 2016
Global News

WAZIRI mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau amemshutumu katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon kwa kuunga mkono ugaidi, baada ya kusema kuwa ni jambo la kawaida kwa watu wanaotawaliwa au kukandamizwa, kukabiliana na walowezi.

Hayo yamejiri kufuatia Zaidi ya Wapalestina 155, Waisraeli 28, Mmarekani na Raia wa Eritrea kuuawa kwa kushambuliwa kwa risasi na visu tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban amesema visa hivyo vimeongezeka kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miongoni mwa Wapalestina na hasa vijana.

Comments are closed.