NEWCASTLE YAILAZA NORWICH CITY

NEWCASTLE YAILAZA NORWICH CITY

Like
267
0
Monday, 19 October 2015
Slider

Newcastle hatimaye imeonja ushindi baada ya kuinyuka Norwich city.

Ligi kuu ya soka ya England ilieendelea tena hapo jana kwa mchezo mmoja ambapo New castle United walikuwa wenyeji wa Norwich city katika dimba la St James’ Park.

Katika mchezo huo New castle waliibuka na ushindi mnono wa mabao 6-2, ambapo karamu ya mabao hayo ilihitiishwa na mchezaji Mitrovic dakika ya 64 kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo yanaifanya New castle kukaa katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 6, na huo ni ushindi wa kwanza kwa Timu hiyo tangu msimu huu uanze ikiwa imecheza mechi tisa mpaka sasa, imedroo mechi 3, imepotezamichezo 5 na imejikusanyia jumla ya pointi 6 .

Ligi hiyo itaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja ambapo Swansea city watakuwa wenyeji wa Stoke City.

Comments are closed.