NGASA KUIAGA YANGA!!!

NGASA KUIAGA YANGA!!!

Like
595
0
Wednesday, 18 March 2015
Slider

Hatuwezi kumzuia Ngasa kuiaga Yanga kama atapata timu nje na Tanzania pia ni heri na faraja kwetu kwani lengo ni kukuza mpira wa nyumbani kwa kuona wachezaji wanafika mbali kupitia Yanga

Kama ataona amepata nafasi ya kusonga mbele sisi hatuna kipingamizi kwani mpira ni biashara

Hayo yamesemwa na afisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Mulo alipohojiwa kupitia kipindi cha Sport Headquarters

Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu wa ligi na tayari tumeanza mazungumzo nae ila hatutamlazimisha kubaki Yanga iwapo atapata timu nyingine.

Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa mchezaji huyo kwa sasa anampango wa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Jangwani pindi atakapomaliza mkataba wake.

Yanga leo itashuka dimbani kwenye mchezo wa ligi kuu ambapo kikosi hicho kitashuka dimbani kumenyana na Kagera kwenye uwanja wa taifa, Yanga itaingia kwenye mchezo huo huku ikiwakosa nyota wake kadhaa akiwemo nahodha wake Nadir haroub cannavaro kutokana na sababu mbalimbali

 

Comments are closed.