NHIF YAINGIA MKATABA NA JWTZ

NHIF YAINGIA MKATABA NA JWTZ

Like
638
0
Tuesday, 18 August 2015
Local News

MFUKO wa Taifa  wa Bima ya Afya –NHIF, umeingia mkataba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania –JWTZ, ambapo wanachama wa mfuko huo na wategemezi wao watapata huduma za matibabu katika hospitali  za jeshi nchini kote.

Mkataba huo wa miaka mitatu unalenga kupanua wigo wa vituo vya matibabu na kuanzisha ushirikiano wa kihistoria baina ya pande hizo mbili.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo, Mkuu wa Huduma za Afya Jeshini Brigedia DENIS RAPHAEL JANGA, amesema amepokea kwa furaha mkataba huo kwani utawapa nafasi ya kutoa huduma bora kwa kundi kubwa la wanachama wa NHIF ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma katika vituo vya jeshi vilivyo karibu nao.

NHIF2

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini Brigedia Denis Raphale Janga wakikabidhiana mkataba.

Comments are closed.