NHIF YANYAKUWA TUZO 3 ZA UBUNIFU BARANI AFRIKA

NHIF YANYAKUWA TUZO 3 ZA UBUNIFU BARANI AFRIKA

Like
343
0
Tuesday, 16 December 2014
Global News

SHIRIKISHO la Kimataifa la Taasisi za hifadhi ya jamii-ISSA,l imekuwa na utaratibu wa kushindanisha mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye masuala ya ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo uboreshaji wa huduma, uwekezaji, uhamasishaji wa afya sambamba na uepushaji wa hatari makazini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano uliowashirikisha waandishi hao kuhusu tuzo za ubunifu barani Afrika zilizotolewa na shirikisho hilo kwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo HAMISI MDEE amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mpaka sasa umeshinda tuzo 8 ikiwemo tuzo ya ubunifu ya kuboresha huduma ya mawasiliano kwa wanachama kupitia siku ya wadau- CLIENTS’ DAY.

Amebainisha kuwa kwa mwaka huu mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeshinda tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya jamii barani Afrika kwenye sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika mjini Casablanca-Morocco Disemba mwaka huu.

 

 

Comments are closed.