Ni nchi ngapi bado zinatekeleza adhabu za kifo?

Ni nchi ngapi bado zinatekeleza adhabu za kifo?

Like
618
0
Monday, 15 October 2018
Global News

Inadaiwa kuwa inawezekana mataifa 170 wameachana na adhabu hiyo ya kifo au wameanzisha mbadala wa adhabu hiyo.

kwa mujibu wa Amnesty International mwaka 2017, nchi 142 wameacha kutoa hukumu ya kifo kisheria na kiutekelezaji

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo na kusifia jitihada ambazo mataifa mbalimbali wamezichukua ili kutokomeza adhabu hiyo.
Alisema “mataifa 170 inawezekana wameacha kutoa hukumu ya kifo au wameanzisha mbadala wa adhabu hiyo.

Makubaliano ya kusitisha sera au utekelezaji

Ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu hukumu ya kifo imewasilishwa katika tume ya haki za binadamu mwezi septemba mwaka huu na kusema kuwa kuna mataifa 170 wameachana na adhabu hiyo ya kifo kisheria na utekelezaji au hajauliwa mtu kwa zaidi ya miaka 10.

Umoja wa mataifa ambayo ina wanachama 193, hivyo ni mataifa 23 tu ndio ambayo inawezekana walitoa hata hukumu moja ya kifo katika muongo uliopita.

Umoja wa mataifa unasema pia kuwa takwimu hizo zinajumuisha taarifa ambazo wamezipata kutoka nchi wanachama pamoja na asasi za kiraia.

Hata hivyo ,Amnesty inasema kuwa ni mataifa 142 ambayo inawezekanakuwa wameachana na hukumu ya kifo na ndani ya miaka mitano iliyopita,mataifa 33 wametekeleza hukumu hiyo ya kifo hata kwa mtu mmoja.

 

Amnesty inakusanya takwimu zake kwa kutumia takwimu rasmi, ripoti za vyombo vya habari na taarifa zilizotolewa kutoka kwa watu waliohukumiwa kifo na familia zao na wawakilishi.

Nchi nne zilitekeleza mauaji kwa asilimia 84 mwaka 2017(Saudi Arabia, Iraq, Pakistan na Iran). Idadi hiyo haijajumuisha China ambapo takwimu zake ni siri ya taifa hilo. Amnesty inakadiriwa kutoa hukumu ya kifo kwa maelfu ya watu kila mwaka.

Njia ambazo zimetumika kutekeleza adhabu hiyo mwaka 2017 ilikuwa ni pamoja na kupigwa, kunyongwa, kuchomwa sindano na kupigwa risasi.

Shirika la haki za binadamu imerikodi idadi ya hukumu ya vifo 2,591 katika nchi 53 katika mwaka 2017.Lakini katika baadhi nchi, kesi hizo za hukumu hizo za kifo huwa zinabadilishiwa adhabu labda kwa mtu kuwekwa miaka mingi gerezani.

 

cc: BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *