MAHAKAMA moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram.
Wanajeshi hao ambao walipatikana na kosa la uasi,walituhumiwa kukataa kuikomboa miji mitatu iliyokuwa imetekwa na Boko Haram mwezi Agosti.
Wakili wa wanajeshi hao 54 amesema kuwa watawauwa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru.
Hata hivyo Wanajeshi hao wamelalamika kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na kundi hilo la Boko Harm.
Kundi hilo limekuwa likipigana tangu mwaka 2009 na linalenga kujenga nchi inayoongozwa na sheria za Kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi wote walikataa mashtaka na hukumu hiyo inasubiri idhini ya maafisa wa ngazi za juu.
Zaidi ya watu 2,000 wameuwawa katika mashambulizi yaliyolaumiwa kufanywa na kundi hilo.