NIGERIA: BUHARI AONGOZA MATOKEO YA AWALI

NIGERIA: BUHARI AONGOZA MATOKEO YA AWALI

Like
252
0
Tuesday, 31 March 2015
Global News

MATOKEO ya awali ya kura zilizopigwa siku ya Jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa Kiongozi wa upinzani MUHAMMADU BUHARI anaongoza kwa zaidi ya Kura Milioni Mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni Rais GOODLUCK JONATHAN.

Generali BUHARI wa chama cha All Progressives Congress -APC anaonekana kupata matokeo mazuri mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos.

Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao.

Comments are closed.