NIGERIA: JESHI LAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA PUNDA NA FARASI

NIGERIA: JESHI LAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA PUNDA NA FARASI

Like
468
0
Tuesday, 08 September 2015
Global News

JESHI la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, kama sehemu ya juhudi za vita dhidi ya Boko Haram.

Imebainika kuwa Kundi hilo limekuwa likitumia farasi kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanavijiji huku jeshi la Nigeria likionekana kupata mafanikio katika vita vyake dhidi ya Boko Haram.

Taarifa zinasema kuwa tayari kumepigwa marufuku kwa matumizi ya pikipiki ambazo zilikuwa zikitumiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwasafirisha wapiganaji wake katika mashambulizi.

Comments are closed.