NIGERIA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI LEO JIONI

NIGERIA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI LEO JIONI

Like
330
0
Monday, 30 March 2015
Global News

ZOEZI la kuhesabu kura linaendelea nchini Nigeria katika uchaguzi wa rais na wabunge ambao ulifanyika siku ya Jumamosi na jana Jumapili.

Kwa kiasi kikubwa uchaguzi ulifanyika kwa amani, licha ya mashambulizi kadhaa katika eneo la kaskazini, ambayo kundi la Boko Haram limeshutumiwa kuyafanya huku kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Nigeria, Muhammadu Buhari, akitarajiwa kumpa changamoto kubwa rais wa sasa Goodluck Jonathan katika uchaguzi huo.

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa urais nchini humo leo jioni.

Comments are closed.