NIGERIA: RAIS WA BUNGE LA SENETI ATINGA KORTINI

NIGERIA: RAIS WA BUNGE LA SENETI ATINGA KORTINI

Like
224
0
Tuesday, 22 September 2015
Global News

RAIS wa Bunge la Seneti nchini Nigeria, Bukola Saraki leo amefika kortini mjini Abuja ambako anakabiliwa na makosa 13 yanayohusu maadili.

Makosa hayo ni pamoja na kuwahadaa wananchi kwa kigezo cha kutangaza mali yake pamoja na kukosa kutangaza mkopo, makosa ambayo ameyakanusha.

Kesi dhidi yake inaendeshwa na jopo la mahakama kuhusu maadili na inahusu makosa anayodaiwa kuyatenda alipokuwa gavana wa jimbo la Kwara kati ya mwaka 2003 na 2011.

Comments are closed.