NIGERIA YATUMIWA UJUMBE KUSIMAMIA UCHAGUZI

NIGERIA YATUMIWA UJUMBE KUSIMAMIA UCHAGUZI

Like
315
0
Friday, 30 January 2015
Global News

MWENYEKITI wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Nkosazana Dlamini-Zuma ameidhinisha kutuma ujumbe wa waangalizi wa umoja huo nchini Nigeria ili kusimamia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu.

Taarifa kutoka Umoja wa Afrika zimesema kabla ya waangalizi 50 wa muda mfupi wa Umoja huo kwenda Nigeria, umoja huo utatuma wataalam 15 kuwa waangalizi wa muda mrefu, ambao watakuwepo nchini humo hadi tarehe 11 Machi ili kuangalia vipindi mbalimbali vya mchakato wa uchaguzi

Comments are closed.