Nikki Haley ajibu tuhuma za Iran, kuwa Marekani ilihusika na shambulio

Nikki Haley ajibu tuhuma za Iran, kuwa Marekani ilihusika na shambulio

Like
548
0
Monday, 24 September 2018
Global News

Balozi wa Marekani umoja wa mataifa ameitaka Iran ijiangalie yenyewe katika shambulio la la kijeshi lililoua watu 25 siku ya Jumamosi.

Balozi huyo Nikki Haley amejibu tuhuma za rais wa Iran, anayeilaumu Marekani kwa kuhusika na shambulio hilo na kusema kuwa Marekani imewagandamiza watu wake kwa muda mrefu sasa”.

Makundi mawili yamedai kuhusika na shambulio hilo licha ya kutowasilisha ushahidi wao.

Watu wanne waliokuwa na bunduki walishambulia wanajeshi wa mapinduzi ya Iran Kusini Magharibi mwa mji wa Ahvaz siku ya jumamosi na kuua watu 25 ambao ni wanajeshi pamoja na raia akiwemo msichana mdogo wa miaka mine waliokuwa wakiangalia maadhimisho ya gwaride la kumbukumbu ya mapinduzi ya kijeshi ya Iran.

Makundi yanayoipinga serikali ya Iran ya Ahvaz National Resistance na Islamic State (IS) yote mawili yamejinasibu kwa kuhiska na shambulio hilo la mauaji.

Katika mkanda wa video uliooneshwa na kundi la Islamic State, unaoonesha watu watatu wakiwa katika gari wakiwa wamevalia sare za wanajeshi wa jeshi la mapinduzi ya Iran wakielekea kutekeleza shambulio hilo,ingawa wanaume hao katika mkanda huo wa video hawakujitambulisha kama ni kundi la IS lakini walisikika wakihamasisha umuhimu wa jihad

Rais Rouhani huku akiita Marekani kama nchi kandamizi,amesema kwa kushirikana na washirika wake wa nchi za kiarabu wameshirikiana katika kulihsmbulia jeshi la Iran.

Marekani imekanusha kuhusika na shambulio hilo na kusema inalaani mashambulio yote ya kigaidi huku afisa mmoja wa ngazi za juu katika nchi ya falme za kiarabu akisema Rouhani hana ushaidi juu ya lawama zake.

“Amewabana watu wa Iran,watu wanampinga kwa sababu kila pesa inkwenda kwa wanajeshi wake,amekuwa akiwakandamiza watu wake kwa muda mrefu anachojali yeye ni jeshi tu, Haley ameiambia CNN.

“Anaweza kutulaumu atakavyo lakini jambo kubwa analopaswa kufanya ni kujitazama kwenye kioo.”

Kabla ya kuondoka katika mkutano wa umoja wa mataifa mjini New York siku ya Jumapili Rouhani aliapa kuwa kamwe nchi yake haitavumilia uhalifu wa aina yoyote”.

“Ni wazi kuwa tunamjua nani muhusika wa uhalifu huu na wakina nani walihusika kutekeleza unyama huo,”alisema.”

Aidha Rais Rouhan amezilaumu nchi za kiarabu kwa kuwaunga mkono wahalifu kwa kuwapatia msaada wa kifedha,sila na masuala ya kisiasa.

Ameongeza kuwa: “Nchi vibaraka katika ukanda huo hupata msaada kutoka Marekani na nchi hiyo huwalazimisha kufanya inachokitaka kwa maelekezo maalum.”

Ingawa Rouhani hakuzitaja nchi hizo alizoziita kama vibaraka wa Mareekani lakini maoni yake yanazilenga nchi za Saudi Arabia, Falme za Kiarabu UAE na Bahrain.

Iran kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Saudi Arabia kwa kuunga mkono kundi dogo la wanaharakati wanaotaka kuivuruga nchi hiyo.

Nchi zote hizo zilipigania siasa za ukanda huo wa ghuba kwa miongo kadhaa na kuingia katika vita vya kisisa na kidini na kujiingiza katika migogoro ya nchi za Yemen and Syria,ambapo nchi ya Irani ikiwa na idadi kubwa ya waislam wa Kishia huku Saudi Arabia ikiwa na nguvu kubwa ya wasuni walio wengi .

Pia Iran inailaumu Israel kwa kuwaandaa wanaume waliokuwa na bunduki katika shambulio hilo na kusema kuwa nchi hiyo imekuwa ikitamani kukalia ardhi ya waislam kwa mabavu kwa kuzitishia serikali hizo.

Pia siku ya jumamosi Rouhan alitoa lawama kwa wanadiplomasia wa Uingereza,Uholanzi na Denmark kwa kuyapa nguvu makundi pinzani ya nchi yake.

Pande hizo mbili kwa miongo kadhaa zimekuwa katika uhusiano mbaya ambapo Marekani imekuwa ikiilaumu Iran kwa kwa kuzalisha silaha za kinyuklia jambo ambalo Iran imekuwa ikilakanusha ziku zote.

Mwaka 2015, chini ya utawala wa Rais wa Marekani Barrack Obama walipata muafaka juu ya kuzitishwa kwa mradi wa utengenezaji wa sialaha hizo na mkataba huo kusainiwa China,Urusi,Uingereza,Ufaransa na Ujerumani ambapo Iran ilitaka kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi.

Aidha baada ya Rais Donald Trump kuingia madarakani na kutengua makubaliano hayo na kuiwekea Iran vikwazo vipya, na kusema kuwa yoyote atakayefanya biashara na Iran akizinyoonyeshea kidole Urusi na China kuwa nazo zitaadhibiwa.

Rais Trump akiongoza mkutano wa baraza la uasalama la umoja wa mataifa alisema kuwa mkutano huo utajielekeza zidi katika kuingalia Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *