NJOMBE: UONGOZI WA HOSPOTALI YA HALMASHAURI UMEPEWA SIKU 90 KUREKEBISHA MAPUNGUFU YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

NJOMBE: UONGOZI WA HOSPOTALI YA HALMASHAURI UMEPEWA SIKU 90 KUREKEBISHA MAPUNGUFU YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Like
378
0
Monday, 15 February 2016
Local News

UONGOZI wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, vinginevyo  hospitali hiyo itafungwa.

 

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na viongozi, Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.

KIGWAAA

Dkt. Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali, vituo vya afya na zahati anayoifanya ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali.

Comments are closed.