NKURUNZIZA AHAIRISHA UCHAGUZI BURUNDI

NKURUNZIZA AHAIRISHA UCHAGUZI BURUNDI

Like
255
0
Wednesday, 20 May 2015
Global News

RAIS wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .

Sababu ya hatua hiyo ni mgogoro wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo ndogo ya eneo la  maziwa makuu.

Msemaji wa rais  huyo, Willy Nyamitwe ameliambia Shirika la habari la Reuters, kwamba Rais Nkurunziza amechukua uamuzi huo baada ya kupendekezwa na tume ya uchaguzi na kufuatia pendekezo kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na Jumuiya ya kimataifa kutaka uchaguzi uahirishwe.

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa kitisho cha kuzuka machafuko dhidi ya mhula wa tatu wa rais Nkurunziza kimepelekea zaidi ya waburundi laki moja kukimbilia katika nchi jirani za Rwanda,Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Tanzania.

 

Wapinzani wa rais Nkurunziza wanasema kuwa kutangaza kwake nia ya kuwania muhula wa tatu unakiuka sheria na makubaliano ya amani ya mwaka wa 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 13.

 

Nkurunziza kwa upande wake anashikilia kuwa ana haki ya kuwania muhula mwingine kwani muhula wa kwanza hakuchaguliwa na wanainchi bali wabunge.

Comments are closed.