NKURUNZIZA AJIANDAA KUGOMBEA MUHULA WA TATU BURUNDI

NKURUNZIZA AJIANDAA KUGOMBEA MUHULA WA TATU BURUNDI

Like
257
0
Wednesday, 15 July 2015
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amefanya mazungumzo ya upatanishi nchini Burundi huku rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza akijiandaa kugombea muhula wa tatu madarakani licha ya kuwepo kwa machafuko ya wiki kadhaa sasa yanayoipinga hatua yake hiyo.

Museveni alikutana jana jioni na wajumbe wa serikali na viongozi wa upinzani mjini Bujumbura.

Burundi imekuwa katika mgogoro wa kisiasa tangu mwezi Aprili mwaka huu baada ya chama tawala cha CNDD-FDD (cndede –fdede) kumteua rais Nkurunziza kama mgombea rasmi wa urais kwa muhula wa tatu mfululizo.

Comments are closed.