NKURUNZIZA ATOA ONYO LA MWISHO KWA WAPINZANI

NKURUNZIZA ATOA ONYO LA MWISHO KWA WAPINZANI

Like
254
0
Tuesday, 03 November 2015
Global News

WAKATI Burundi ikiendelea kukabiliwa na ghasia kutoka wa upinzani baada ya kuchaguliwa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuongoza kwa mhula wa tatu katika mazingira yenye utata, rais huyo ametoa ilani ya mwisho kwa wale aliowataja kuwa watenda mabaya kujisalimisha.

Katika hotuba yake kwa Taifa, Nkurunziza amesema kuwa wale ambao hawatajisalimisha katika kipindi cha siku tano zijazo watashtakiwa kama maadui wa Taifa.

Hayo yamejiri wakati mauaji yakiendelea kuripotiwa katika mji mkuu wa Bujumbura ambapo watu kadhaa wameuwawa kutokana na milipuko.

Comments are closed.