NOVAK DJOKOVIC ATUPWA NJE KWENYE MICHUANO YA WAZI YA QATAR

NOVAK DJOKOVIC ATUPWA NJE KWENYE MICHUANO YA WAZI YA QATAR

Like
264
0
Friday, 09 January 2015
Slider

Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic ametupwa nje katika michuano ya wazi ya Qatar baada ya kupokea kichapo ca seti 6-7 (2-7) 7-6 (8-6) kutoka kwa Ivo Karlovic.

Djokovic ambaye alijitoa katika michuano iliyopita alionekana anashindwa kuendana sawa na kasi ya mkongwe huyo kutoka katika taifa la Croatia mwenye umri wa miaka 35.

Kwa matokeo hayo sasa Ivo atacheza na raia wa Hispania, David Ferrer aliyefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa kumtoa Dustin Brown kwa seti 6-2 6-2.

Katika mchezo mwengine wa nusu fainali utawakutanisha Tomas Berdych dhidi yaAndreas Seppi.

Comments are closed.