NYALANDU ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI

NYALANDU ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI

Like
338
0
Wednesday, 15 July 2015
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi-CCM.

Nyalandu amechukua fomu hiyo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia kazini baada ya kutoka kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.

Nyalandu anaimani kwamba akisimama kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo atashinda kwani ana vigezo vyote vinavyostahili kumpa nafasi hiyo lakini pia amewataka watanzania kuwa na imani naye.

Comments are closed.