NYALANDU: TUKIEPUKA MISUGUANO TUTALINDA HIFADHI ZETU AFRIKA MASHARIKI

NYALANDU: TUKIEPUKA MISUGUANO TUTALINDA HIFADHI ZETU AFRIKA MASHARIKI

Like
249
0
Tuesday, 27 January 2015
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa LAZARO NYALANDU amezitaka nchi zinazopakana na Tanzania na zinazoshirikiana katika suala la Utalii kutumia zaidi njia ya Majadiliano kuepuka misuguano isiyo ya lazima

Mheshimiwa NYALANDU ametoa rai hiyo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake wakati akizungumzia msuguano uliojitokeza na nchi za Kenya baada ya magari ya Tanzania ya kubeba Watalii kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta.

Magari hayo yanayotokea katika jiji la Arusha na Moshi yalizuiwa kuingia nchini humo kwa takribani wiki mbili hali iliyosababisha usumbufu wa abiria na Watalii.

Comments are closed.