NYAMAGANA: WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPYA TARATIBU ZA UTOAJI WA HUDUMA YA AFYA

NYAMAGANA: WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPYA TARATIBU ZA UTOAJI WA HUDUMA YA AFYA

Like
267
0
Tuesday, 10 November 2015
Local News

BAADHI ya wazee wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza wameiomba serikali kuangalia upya utaratibu wa utoaji huduma za Afya katika hospitali ya wilaya hiyo kwani haukidhi mahitaji.

Wakizungumza na Efm wazee hao wamesema kuwa tangu utaratibu wa kutolewa huduma bure kwa wazee uanze  suala hilo limekuwa ni kitendawili kwao  kutokana na kutopatiwa huduma hiyo kama inavyoelekezwa.

Aidha wamesema kuwa serikali imefanya suala zuri la kuanzisha dirisha maalumu kwa ajili yao lakini utaratibu huo kwa baadhi ya hospitali na zahanati bado haujawa mzuri na kumwomba Raisi wa awamu ya tano dokta John Pombe Magufuli kuliangalia  suala hilo.

Comments are closed.