Nyota Ndogo alizwa na historia ya mama yake, Aomba msaada kwa Watanzania

Nyota Ndogo alizwa na historia ya mama yake, Aomba msaada kwa Watanzania

Like
832
0
Monday, 26 March 2018
Music

Nyota Ndogo

Nyota Ndogo

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nyota Ndogo amewaomba wana Afrika Mashariki kumsaidia kutafuta ndugu wa mama yake mzazi ambao hadi leo hii hawajui walipo.

Nyota Ndogo amesema kuwa mama yake mzazi alifika nchini Kenya akitokea Zambia akiwa na miaka 14 akisafirishwa na rafiki na baba yake (Babu wa Nyota Ndogo) kwa lengo la kwenda kusoma.

Nyota Ndogo amesema kuwa mama yake hakufanikiwa kwenda shule kama alivyoahidiwa bali aliishia kuwa kijakazi wa nyumbani.

Baadaye Mama yake alipata bahati ya kuolewa na mwanaume kutoka Tanzania ambaye ndio baba yake mzazi, na kwa maelezo ya mama yake kwenye familia yao walizaliwa watoto 15 na mama yake alikuwa ndiye mtoto wa mwisho.

“Anatokea Zambia kisha baba anatokea Tanzania lakini sisi tumezaliwa pale makadara hospital. Mimi ni 001 damu kisha my mum alitoka kwao akiwa 14 years but kasahau kikwao. hatujui mtu hata mmoja wakutoka upande wa mama, anasema kwa wapo kumi na tano na yeye ndio alikua wa mwisho hajui kama babake yupo au hayupo anasema anatokea Tunduma.“ameandika Nyota Ndogo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande mwingine Nyota Ndogo amesema kuwa kwa sasa anahitaji kufanya ziara nchini Tanzania maeneo ya Tunduma, ambapo amesema kuwa anachohitaji kutoka kwa watu wa Afrika Mashariki ni kumsaidia kutambua lugha anayozungumza mama yake ili apate wepesi wa kutafuta ndugu wa mama yake.

“Nataka kufanya tour ya kumtafutia familia yake alikuja vipi Kenya? Rafiki ya babake alikwenda kumchukua kwa wazazi wake nakusema anakuja kumsomesha badala yake akamgeuza kijakazi,” ameeleza Nyota Ndogo.

Baba mzazi wa Nyota Ndogo ni Mtanzania lakini kwa upande wa mama yake bado haijajulikana asili yake ingawaje wameishi Kenya kwa muda mrefu.

 

Comments are closed.