NYUMBA MILIONI MOJA KUPATIWA UMEME WA SOLA IFIKAPO MWAKA 2017

NYUMBA MILIONI MOJA KUPATIWA UMEME WA SOLA IFIKAPO MWAKA 2017

Like
228
0
Monday, 16 February 2015
Local News

SERIKALI ya Tanzania imesema hadi ifikapo mwaka 2017, itakuwa imetimiza mpango mahususi wa kutumia umeme wa sola uitwao ‘One Solar Homes’ katika nyumba milioni moja.

Akizungumza Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, LUTENGANO MWAKAHESYA, amesema mradi huo unatarajia kutoa huduma ya umeme kwa Asilimia 10 ya watu nchini na ajira 15000 zitakazohusu sola.

Amebainisha kuwa mpango huo ni mfano mzuri kwa Mataifa mengine ambayo yana malengo sambamba na mradi wa Power Afrika Initiative uliotangazwa na Rais wa Marekani BARACK OBAMA mwaka 2013, wenye malengo ya kufikisha umeme kwa nyumba Milioni 60 Barani Afrika.

Comments are closed.