OBAMA AANZA ZIARA YA KIHISTORIA CUBA

OBAMA AANZA ZIARA YA KIHISTORIA CUBA

Like
214
0
Monday, 21 March 2016
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba, akiwa ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Taifa hilo katika kipindi cha miaka 88 iliyopita.

Ziara hiyo ya siku tatu ndiyo kilele cha mazungumzo ya miaka miwili yaliyonuia kurekebisha uhusiano kati ya Marekani dola kubwa zaidi duniani na jirani yake yenye mfumo wa ujamaa.

Katika ziara yake Rais Obama atakutana na Rais wa Cuba Raul Castro Pia ameahidi kuangazia masuala ya haki za binadamu, kuwepo mageuzi ya kisiasa ingawa maafisa wa Cuba wamesema hakuna ajenda ya kujadili juu ya nchi hiyo kukubali mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Comments are closed.