OBAMA AISIHI UINGEREZA ISIJITOE EU

OBAMA AISIHI UINGEREZA ISIJITOE EU

Like
285
0
Friday, 22 April 2016
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza kubaki katika jumuiya ya Umoja wa Ulaya ili kuweza kuchangia katika vita dhidi ya ugaidi na masuala ya wahamiaji na utatuzi wa migogoro ya kiuchumi.

Rais Obama amenukuliwa na gazeti la Uingereza la Telegraph, akisema kwamba uanachama wa Uingereza katika umoja wa Ulaya una umuhimu mkubwa na endapo nchi hiyo itajiondoa katika umoja huo itapunguza nguvu katika vita dhidi ya ugaidi duniani.

Hata hivyo Obama amesema anatetea hoja ya umoja wa Ulaya kuendelea kama ulivyo badala ya Uingereza kujitoa ingawa anakabiliwa na upinzani kutoka kwa viongozi wa juu wa Uingereza wanapiga kampeni kujitoa katika umoja huo.

Comments are closed.