OBAMA AITAKA IRAN ISITISHE MPANGO WA NYUKLIA

OBAMA AITAKA IRAN ISITISHE MPANGO WA NYUKLIA

Like
236
0
Tuesday, 03 March 2015
Global News

RAIS wa Marekani BARACK OBAMA ameihimiza Iran isitishe mpango wake wa nyuklia angalau Muongo Mmoja, kama sehemu ya Mkataba unaotarajiwa kufikiwa kulegeza vikwazo.

Kauli ya Rais OBAMA imekuja kabla hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel BANJAMIN NETANYAHU katika bunge la Marekani leo kupinga mkataba huo.

Bwana OBAMA amesema Iran itahitaji kukubali mkataba utakaositisha uwezo wake wa kurutubisha Madini ya Urani na kuweka chini ya kiwango kinachohitajika kutengeneza Silaha za Nyuklia.

Comments are closed.