RAIS wa Marekani BARACK OBAMA amesema hakubaliani na uamuzi wa Jaji wa Mahakama nchini humo wa kusitisha utekelezaji wa amri yake ya utendaji kuhusu mageuzi ya uhamiaji.
Bwana OBAMA amesema sheria hiyo na historia viko upande wa utawala wake.
Wizara ya Usalama wa Ndani wa nchi hiyo imesema itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama na kwamba utawala umechukua mwelekeo mzuri kwa mujibu na utawala wake wa sheria, lakini imeeleza kuwa kwa sasa itabidi ikubaliane wa uamuzi wa mahakama.