OBAMA ATAJA SHAMBULIO LA CALIFORNIA KUWA NI LA KIGAIDI

OBAMA ATAJA SHAMBULIO LA CALIFORNIA KUWA NI LA KIGAIDI

Like
190
0
Monday, 07 December 2015
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amelihutubia Taifa lake kufuatia shambulio la risasi la wiki iliyopita katika jimbo la California ambalo lilisababisha vifo vya watu 14.

Rais Obama amesema wazi kuwa hakuna ushahidi kwamba mhusika alikuwa anatekeleza mauaji hayo kwa maelekezo ya kundi lolote kutoka nje ya Marekani.

Katika hotuba yake amesema kwamba shambulio hilo lilikuwa la kigaidi hivyo ni muhimu kupambana nalo bila kuchukua sura ya vita baina ya Marekani na waislamu bali ni kwa waislamu wenye itikadi kali za kigaidi.

Comments are closed.