OBAMA ATARAJIWA KUTUA KENYA LEO

OBAMA ATARAJIWA KUTUA KENYA LEO

Like
237
0
Friday, 24 July 2015
Global News

RAIS Barack Obama wa Marekani yuko njiani kuelekea Kenya hii leo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza akiwa rais kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki, alikozaliwa baba yake mzazi.

Obama, ambaye ni rais wa kwanza mweusi nchini Marekani, ni mtoto wa Barack Hussein Obama Mkubwa, Mkenya aliyekutana na mama yake Obama, wakati wawili hao wakisoma nchini Marekani.

Anatazamiwa pia kukutana na baadhi ya jamaa zake wa ubabani akiwa Nairobi, ingawa hategemewi kutembelea kijiji cha Kogelo inakotokea familia yake.

Comments are closed.